Congratulations Joyce & Jorge

0

Mungu awaongoze njia za kupita katika ndoa yenu. Pendaneni na msameheane bila kujali ukubwa wa tatizo. Salini kwa pamoja, muwekeni MUNGU mbele katika kila jambo.

Nawapenda sana.

0 comments:

CCM HOUSTON; SHEREHE YA USHINDI WA RAIS MAGUFULI

0

Wana Houston wakishereheka kwa pamoja kufuatia ushindi wa aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi, CCM,  Muheshimiwa ndg John Pombe Magufuli, Rais Magufuli alikwisha apishwa tarehe 5 mwezi 11,2015.

Sherehe za kuapishwa Rais Magufuli zilifanyika jijini Dar es salaam, Tanzania. Marais kutoka nchi mbalimbali walihudhuria tukio hilo.

Kwa sasa Rais Magufuli kashaanza kazi kwa vitendo, amefuta safari zote za kwenda kutembea nchi za nje, yeye ni kazi tu, (HAPA NI KAZI TU) huo ni msemo wake mkuu ambao alikuwa akiutumia mara kwa mara  wakati akifanya kampeni zake za kiti cha urais katika miji  mbalimbali nchini Tanzania.

MUNGU ambariki Rais Magufuli aendelee kufanya kazi zake kwa vitendo kwa kipindi chote cha urais wake.0 comments: