Umeshaisikia Hii ya Diamond na Irene Uwoya??

0

Habari zilizotapakaa leo kwenye magazeti mbalimbali ya udaku nchini zinaongelea juu ya tukio linaloonekana kama fumanizi kati ya mwigizaji mahiri wa bongo movies Irene Uwoya na Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul maarufu kama “Diamond platnumz” katika hoteli moja ya kifahari huko mitaa ya mbezi jijini Dar es salaam.

Picha za habari hizo zinaonesha wawili hao wakiingia hotelini usiku na kutoka hotelini hapo pamoja mida ya mchana siku inayofuata na pia kuna ushahidi wa magari ya wawili hao yakiwa yamepakiwa hotelini hapo.

Bado tunaendelea kujaribu kufanya mawasiliano na Irene Uwoya ili tuweze kupata ukweli halisi wa tukio hili.


0 comments: