Picha 11 za Miss Tanzania Brigitte akiwa Indonesia tayari kwa ajili ya mashindano ya Miss World 2013

0

Miss Tanzania Brigitte Lymo kwasasa yuko nchini Indonesia kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss World 2013 yanayotarajiwa kufanyika mwezi huu.


Akiwa na Miss Uganda


Miss Switzerland,Slovakia,Turkey,Vietnam,Czech rep,Guyana,Trinidad and Tobago at diinnneerrr 


Miss Trinidad and Tobago, Miss Guyana,Miss Tanzania!




vietnam, malaysia, nicaragua ,uganda, namibia, czech republic


MBUNGE WA CHADEMA BAADA YA KUMPIGA MATEKE ASKARI WA BUNGE NA KUJIFICHA SASA AJISALIMISHA POLISI MWENYEWE!!

0


BAADA ya Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kumsaka
kwa siku mbili bila mafanikio mbunge wa Mbeya
Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Sugu
(CHADEMA), akidaiwa kumpiga na kumjeruhi mmoja
wa askari wa Bunge, hatimaye alijisalimisha
mwenyewe jana jioni.
 
Taarifa zilizotufikia wakati tunakwenda mitamboni,
Sugu alikwenda polisi akiongozana na Mwenyekiti
wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na wabunge Tundu
Lissu (Singida Mashariki), John Mnyika (Ubungo) na
Joshua Nassari (Arumeru Mashariki).
Akizungumza na mwandishi wetu, Mnyika alisema
kuwa Sugu hakukamatwa bali alijipeleka mwenyewe
polisi kwa hiari yake na kwamba jioni hiyo majira ya
saa 1:10 alikuwa akiandikisha maelezo yake.
 
Wakati Sugu akijisalimisha, wanasheria wa Bunge
nao walikuwa wamejifungia kuangalia namna ya
kumkabidhi mbunge huyo mikononi mwa sheria.
Juzi na jana viwanja vya Bunge vilitawaliwa na idadi
kubwa ya polisi waliotumwa kumkamata Sugu lakini
mpaka Bunge linaahirishwa jioni haikujulikana ni
wapi alikokuwa mbunge huyo.
Mbunge huyo juzi baada ya kubebwa mzobemzobe
na askari wa Bunge na kisha kutolewa nje ya ukumbi,
inadaiwa kuwa alimpiga ngumi mmoja wa askari
aliyemtuhumu kuwa alikuwa amempia ngumi wakati
wakimtoka nje.
 
Askari hao juzi jioni walikuwa kwenye vikundi
vikundi nje ya ukumbi wa Pius Msekwa ambako
kulikuwa kukifanyika mkutano wa wabunge wa
upinzani ambapo Sugu pia alikuwa miongoni mwao.
Kutokamatwa kwa Sugu kumewashangaza wengi
waliokuwa karibu na askari hao kwa kuwa alikuwa
amekaa jirani nao akizungumza na wenzake kabla ya
kuanza kwa kikao chao.
 
Tanzania Daima lilidokezwa kuwa askari hao
walishindwa kumkamata Sugu kwa kuwa
hapakuwepo na amri ya kukamatwa kwake na hata
ilipotolewa alikuwa ameshaondoka katika viwanja
vya Bunge.
 
Mpaka Bunge linaahirishwa juzi jioni, idadi kubwa ya
askari walikuwa nje ya milango na korido zilipo ofisi
za kambi ya upinzani wakimsubiri Sugu bila
mafanikio.
 
Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa miongoni mwa
mambo yaliyochangia askari kusuasua kukamatwa
kwa Sugu ni kutokana na kinga ya kibunge aliyonayo
na pia kosa analotuhumiwa kulifanya alilifanya akiwa
kwenye viwanja vya Bunge.
 
“Tulipata mtanziko wa kumkamata haraka haraka,
ilibidi lazima tuwasiliane na ofisi ya Spika kujua
taratibu za kumkamata kiongozi huyo hasa kwa kuwa
alifanya kosa hilo akiwa bungeni,” kilisema chanzo
kimoja.
 
Wakati askari wakihaha kumtafuta Sugu, mbunge wa
Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (CCM), jana
aliomba mwongozo wa Spika kuhusu tukio la vurugu
zilizotokea juzi bungeni hasa tukio la Sugu kumpiga
askari.
 
Sendeka alisema tukio hilo limelidhalilisha Bunge na
askari wanaowalinda, hivyo akataka liweke wazi ni
hatua gani zitakazochukuliwa dhidi ya mbunge huyo
ili kulinda heshima ya chombo hicho.
 
“Nataka nijue ibara ya 100 ambayo humpa kinga
mbunge na uhuru wa mawazo akiwa ndani ya Bunge
inatumikaje katika tukio hili?
“Je, Bunge litalindaje heshima yake dhidi ya tukio hili
lililofanywa na mbunge mwenzetu?” alihoji.
Akijibu mwongozo huo, Mwenyekiti wa Bunge,
Jenister Mhagama, alisema tukio hilo ni geni hivyo
Bunge limeshindwa kutoa jibu la mara moja.
 
“Jambo hili halijawahi kutokea katika historia ya
Bunge, sasa nami nitalifikisha kwa wanasheria wa
Bunge wanishauri namna ya kulishughulikia na
baada ya hapo nitatoa mwongozo,” alisema.
Akitoa mwongozo huo muda mfupi kabla ya Bunge
kuahirishwa jana jioni, Naibu Spika, Job Ndugai,
alisema kuwa bado wanashauriana na wanasheria
kuona kanuni zinawaelekezaje.
 
Alisema kuwa licha ya tukio hilo kutokea katika eneo
la Bunge bado kitendo hicho ni cha jinai na hivyo,
mtuhumiwa atashughulikiwa kisheria.
“Ni sawa na jaji yuko mahakamani ambapo kuna
kinga kama za Bunge halafu jaji mwenzake ampige
ngumi. Huyo lazima achukuliwe hatua hawezi
kuachwa. Kinga zetu ziko kwenye uhuru wa mawazo
tu,” alisema.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, juzi lilitangaza
kumsaka Sugu kwa tuhuma za kufanya vurugu na
kumjeruhi askari wa Bunge.
“Lakini tuna mashaka sana na hatua yake aliyoifanya
nje ya ukumbi ambapo alimvamia na kumpiga ngumi
nzito Koplo Nikwisa Nkisu ambaye alijeruhiwa jicho,”
alisema mmoja wa askari ambaye hakutaka jina lake
litajwe.
 
Ofisa Upelelezi wa Wilaya ya Dodoma ASP Jumanne
Kim, juzi jioni alithibitisha kusakwa kwa mbunge
huyo aliyeondoka maeneo ya Bunge mchana akiwa
ndani ya gari la kiongozi mkuu wa kambi rasmi ya
upinzani bungeni, Freeman Mbowe.

Fashion Week!!

0











Celebs With Style.

0
















BAADA YA DAYNA, BABA LEVO NAE AFUNGUKA NA KUDAI KUIBIWA KORASI YA WIMBO MPYA WA DIAMOND "MY NUMBER ONE"...!!!

0
https://fbcdn-sphotos-a-a.akamaihd.net/hphotos-ak-prn2/q83/1185392_659474667396477_477324071_n.jpg
NARUDIA tena nina asilimia 100 DAIMOND PLATNUM amecopy KORAS yangu coz nimekuwa nikimuimbia kila tunapokutana kwa lengo la kumshirikisha kwenye wimbo wangu (SWEATY SWEATY) ni zaidi ya miezi saba au nane imepita akinizungusha tu.
Na kwa kudhibitisha Hilo mimi nina DEMO 5 za KORASI yangu ambazo nimefanya kwenye studio mbali mbali Ya kwanza 1 kwa MORE FIRE magomeni 2 STUDIO SINZA 3 kwa TUDY THOMAS mbezi 4 kwa G BAKUZA KIGOMA 5 kwa MR T TOUCH mwenge... 
Ninaweza kuwasikilizisha watu demo zote Tano lakini sio kuuachia huo wimbo coz ntaonekana walewale wategemea KICK. wakati MIMI KWA SASA sihitaji kick ya mtu coz msimu huu nina nguvu ya kutosha. na nina jiamini.. ukitaka kuamini angalia kilichotokea FIESTA MTWARA JUZI..

PICHA ZA VURUNGU NA VIMBWANGA VYA BUNGENI!!!

0

21Ni vurugu ambazo zimetajwa kutokea kwa mara ya kwanza kwenye historia ya bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania wakati wa mjadala wa muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba.

22

23

17

13

14

15

12

16

18

24

20

19


Hehehehehee Maana badala ya kusikitika inabidi nicheke!!! What the hell are these people thinking?? Nyerere  would be so disappointed.. 

Picha kwa hisani ya Millard ayo 

PICHA ZA AWALI RAIS KIKWETE NA KAGAME WALIPOKUTANA HII LEO,NI WAZI MAMBO YAPO SHWARI..

0

Rais Poul Kagame wa Rwanda akiteta jambo na Rais Jakaya Kiwete wa Tanzania kulia wakati walipok utana katika mkutano wa ICGLR Summit mjini Kampala Uganda leo.   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Rais Paul Kagame wa Rwanda wakati walipokutana faragha sambamba na mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa Makuu uliofanyika katika Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, jijini Kampala,Uganda. 
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakati walipokutaba na kufanya mazungumzo ya faragha, katika Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, jijini Kampala, Uganda.