kupunguza kitambi
usikimbilie kutatua tatizo tafuta kwanza nini chanzo cha kitambi?
Kilitokana na nini? Anagalia vyakula unavyokula, na staili ya maisha....
kutoa kitambi sio kazi rahisi unatakiwa uwe na nidhamu katikta ukaji na
kufanya mazoezi hakuna shortcut...kwa kuanzia acha tabia ya kunywa maji
ya baridi kila ukimaliza kula baadala yake kunywa ya moto au uvuguvugu.
Maji baridi yanagumisha/ solidfy chakula ulichokula sasa kama umekula
vyakula vya mafuta ndo balaa. Pendelea kunya maji ya uvuguvugu
yaliyotiwa asali kidogo kila asubui kabla hujala bleakfast na usiku..
Puguza kiwango cha sukari unachokula mfano soda na bia,na kwenye chai,
pendelea kula mapema usiku na ulale baada ya masaa mawili au matatu
baada ya kula..mengine google usome mwenyewe we sio mtu wa kwanza kuwa
na kitambi duniani...
1.Ruka kamba sana.
2.Fanya jogging hata ukiwa chumbani kwako waweza fanya (static jog).
3.Punguza kula kula na ukila kula kiasi.
4.Punguza kulala muda mrefu usiku(kama huna cha kufanya chezacheza na shemeji atleast mara moja kila siku.)Nadhani umenielewa.
Afya ya mtu inahusisha Chakula moja kwa moja.
Kuwa na kitambi sio afya, watu wengi wanafikiri mtu mwenye kitambi ni afya.
Kitambi kwa kiingereza ni Obesity.
Matunda na mboga mboga zina umuhimu katika kupunguza kitambi au tumbo kwa wanawake warembo.
Inashauriwa kupunguza kula vyakula vya wanga na mafuta ili kuepuka
uwezekano wa kupata tumbo. Kila mlo unatakiwa uwe na mboga mboga. Pia
usile chakula ukashiba, kula chakula kiasi na jazia kwa matunda.
Usinywe maji wakati wa kula, kunywa maji kabla ya kula haswa lisaa kabla au kunywa maji masaa 2 baada ya kula.
-ULAJI
Ipo mifumo miwili ya kula. Chakula unachokula na namna unavyokila.
Unavyokula.
-Kuna kula vyakula vidogo vidogo vyenye madini, vitamini, mafuta nk
mara nyingi kwa siku; au kula milo michache (mmoja au miwili) mikubwa
ili kujaza tumbo. Ulaji mdogo mdogo husaidia afya na kuingia mwilini
vyema kuliko ulaji mkubwa wa mara chache. Tumbo lina musuli zinazofanya
kazi kama mashine au mnyama. Gari likijaa sana hupata taabu kwenda.
Punda hivyo hivyo. Ulaji mdogo mdogo unaosambazwa mara kadhaa kwa siku
ni bora maana mwili unachambua kila kitu kwa wepesi na haraka. Unapokula milo michache mikubwa unapalilia zaidi mafuta mwili.
(PENDEKEZO la kwanza. Asubuhi, kunywa maji kwanza, matunda, kisha ndiyo chai na vitu vingine kama mkate au maandazi…)
-Wapo wanaodai kwamba wanakula matunda na mboga.
Tatizo ni kwamba mipangilio yao huwa ya makosa. Mathalan wengi hula matunda baada ya chakula.
Vimeng’enya chakula (enzymes) tumboni hufanya kazi namna tofauti.
Mathalan vile vinavyonyambua matunda ni tofauti na vinavyomeng’enya vitu
vigumu zaidi kama nyama au wanga. Matunda hunyambuliwa haraka zaidi
kuliko vyakula vingine. Hivyo ni bora kula matunda dakika10-20 kabla ya
chakula. Ukila baadaye matunda hugeuzwa aina fulani ya pombe (fermented
food) inayoelea tu juu ya chakula na kubakia kitu kingine badala ya
kuingizwa haraka ndani ya damu kupitia utumbo mdogo, uwengu, moyo, ini,
nk.
Tatizo jingine ni kupika sana mboga hadi zikapoteza nguvu.
-Mseto wa vyakula pia ni muhimu. Kwa mfano vyakula vyenye uchachu
(acid) na vile vinavyomumunyuka haraka (alkine) havitakiwi viliwe
pamoja. Mfano ni matunda. Matunda chachu kama machungwa, mananasi na
maembe yatakiwa yawe pamoja; na yale laini zaidi: ndizi mbivu, matikiti
maji, mapapai, matufaha, nk yaende kivyake, maana yana mfumo tofauti,
wa kumeng’enywa.
Mpishi
Patrick Maka ( katikati, akiwa na wenzake kazini Dar) ni kati ya
wapishi wa Kitanzania wanaopigania sana ulaji wa chakula bora
Hali hiyo pia iko katika nyama. Nyama nyeupe (ndege na samaki) tofauti na nyama nyekundu (ng’ombe, kondoo, nk) ziliwe tofauti.
Chakula unachokula
Waafrika hatuna tabia ya kula mboga mboga mbichi. Tunafuata ladha na mazoea kuliko thamani.
Bara letu lina mboga na vyakula bora kuliko bara lolote duniani
lakini sisi tunakufa mapema na kwa utapia mlo kuliko wale wanaotoka nchi
kame. Ulaya nzima imejazana mboga mboga zinazoagizwa toka Afrika. Kenya
na Tanzania zinauza mboga za maharagwe mabichi (green beans), matunda
toka Afrika Kusini na Ivory Coast; nk. Waafrika tunapenda kujaza
matumbo. Unene umekithiri hata wale walio matajiri waliosoma bado
wanakufa kwa kisukari shauri ya kutokula mboga mbichi.
Ulaji wa mboga mbichi ni upi?
Ni mathalani ulaji wa salad. Tanzania tunaita kachumbari. Lakini si
lazima iwe kachumbari ya nyanya, vitunguu na chumvi tu. Waweza
kuchanganya matango, nyanya kwa maparachichi; au vitunguu saumu,
giligilani na karote. Huu mseto wa mboga mbichi ni mzuri ukienda na
chakula chenye nyama za minofu na wanga (ugali, wali, ndizi za kupika
nk). Ulaji wa wanga asubuhi, mchana na jioni kila siku huchangia sana
katika unene.
(PENDEKEZO LA 2. Ugali kwa samaki; mboga ya majani ya matango kwa nyanya. Usiweke chumvi kwenye hiyo mboga mbichi ya majani.)
Majani
na mimea yamezingirwa na barafu Ulaya- vyakula vingi vya watu hawa
huagiziwa na kutegemewa Afrika. Lakini wanakula vizuri kutuzidi.
Kwanini? Picha na F. Macha
2-UNYWAJI MAJI
Waafrika hatunywi maji, hasa wanawake. Wanaokunywa maji zaidi ni
wacheza michezo. Wengi wetu hunywa zaidi soda (vinywaji baridi kama
Cocacola, Pepsi, Mirinda ,Tangawizi na gesi za kisasa kama Red Bull)
zilizojaa gesi inayoleta vidonda tumboni; na chai. Kuliko maji. Na maji
haya hutakiwa dakika 10-20 kabla ya chakula au nusu saa kuendelea baada
ya chakula. Ukila chakula huku unasakatia maji huimanisha mtu una kiu.
Ulaji chakula na unywaji maji ni vitu viwili tofauti. Ila utawaona watu
wanakula huku wakibugia maji. Unapokula chakula huku unabugia maji
unapunguza nguvu za chakula, unajaza tumbo maji na kuchelewesha
mmeng’enyo wa chakula (digestion).
Chakula kisipomeng’enywa vizuri kinaketi tu tumboni. Matokeo wengi
wetu tuna matumbo makubwa. Kama hufanyi mazoezi lile tumbo linakwenda
pembeni (chini ya mbavu) hasa kwa watu wa makamo linaleta maradhi kama
kisukari, kiungulia, kuvimbiwa, uyabisi wa tumbo, nk.
Farasi
ni mnyama asiyeliwa ovyo Uingereza; hufugwa tu kwa kazi na michezo. Ipo
hoteli moja Scotland imeanza kupika nyama yake kwa chips. Imeandamwa
sana na "wapinzani wa kula nyama" wa Kitasha... (Picha na F. Macha)
3-SUALA LA UMENG’ENYAJI
Chakula huanza kumeng’enywa au kusagwa (kwa lugha iliyozoeleka)
mdomoni. Mate yako mdomoni ni chanzo cha uchambuaji chakula. Unapobugia
chakula bila kutafuna sawasawa unasababisha mambo mawili. Moja chakula
kutochambuliwa vizuri, pili chakula kwenda kukaa tu tumboni, au kama
kikipita hakisaidii lolote mwilini. Utafunaji wa taratibu husaidia
umeng’enyaji. Chakula kinapofika tumboni hukaa pale dakika ishirini.
Hapo huchanganywa na asidi (ya manjano iitwayo Hydrochloric)
inayokibadilisha tayari kupelekwa utumbo mkubwa, kupitia kongosho. Kule
uchafu utapelekwa chini na rutuba kusafirishwa na utumbo mdogo kuelekea
katika uwengu, moyo. Moyo utadunda chakula kilichoshageuzwa damu
kuelekea mwilini kufanya kazi na akiba hubakishwa katika ini.
Sasa kama usipotafuna vizuri, ukila huku unakunywa sana maji au
vinywaji vingine chakula hakimeng’enywi vizuri. Ndiyo maana unawaona
watu wengine wanakula sana lakini hawana afya. Wanaugua ovyo ovyo,
wanatoka jasho ovyo, wanajamba ovyo, wana matumbo makubwa, wanavimbiwa,
wanakaa siku nyingi bila kwenda choo (inatakiwa mtu kwenda haja kubwa
mara moja au mbili kwa siku) nk.
Misitu na hewa safi ya mimea- (Picha na F. Macha)
4-ULAJI WA VYAKULA VYA MAFUTA
Mafuta ni suala muhimu sana mwilini. Ila ulaji wake shurti uwe wa
mpangilio. Yaani unaowiana. Lazima mtu uwe na wastani mzuri wa vyakula
vya nguvu, yaani “wanga” (ugali, ndizi, wali, viazi mbalimbali, mikate,
mahindi, nk), ujenzi yaani “protini” (mboga na nyama), “madini” (mbegu
mbegu mbichi si za kukaanga sana na chumvi) na “vitamini” (matunda,
maziwa, mayai, nk).
Waafrika tunapenda nyama. Nyama ni muhimu sana maana ina madini aina
ya chuma (nyama nyekundu) protini,nguvu na mafuta. Ila mafuta yaliyoko
katika nyama mara nyingi si mazuri shauri hayatoki, huganda. Chukua
nyama ya kuku na samaki ambayo huwa na ngozi. Wengi wetu hupenda sana
kula ile ngozi ya wanyama hawa kwa kuwa tamu. Lakini haya ni mafuta
mabaya.
Mafuta ya samaki lakini ni mazuri. Samaki anayo mafuta ya Omega-3 ambayo husaidia mwili na kinga maradhi mwilini.
Tunapokula nyama choma au ya kukaanga, lazima tule pia mboga za
majani (mbichi) na si vizuri kula nyama kila siku. Kama huwezi kukaa
bila nyama kila siku, fanya mazoezi ya mwili.
PENDEKEZO LA 3- Kula mbegu mbegu za korosho, karanga au mlozi
(ziwe mbichi badala ya kukaanga na chumvi) kati kati ya siku. Haya ni
mafuta yenye rutuba mwilini kuliko nyama za mafuta.
Chips za Magimbi zilizopikwa na kuonyeshwa ndani ya tovuti ya
Miriam Rose , dada wa Kibongo anayetukuza mapishi ya Kitanzania
duniani. Habari zaidi tembelea : www.tasteoftanzania.com
5-MAZOEZI YA MWILI NA VIUNGO
Mazoezi ni mfalme wa kupunguza unene.
Ukiwauliza wengi watakuambia wanafanya kazi ngumu za sulubu
(wanachuruzikwa jasho) kwa hiyo hayo ni mazoezi. Ila kazi na mazoezi ni
vitu viwili tofauti. Ingekuwa kufanya kazi ni mazoezi basi kusingekuwa
na wastani mfupi wa maisha kwa maskini hasa sisi Waafrika.
Wengine watadai kwamba walipokuwa wadogo shuleni walifanya mazoezi
sasa wamekuwa watu wazima (miaka 40 kuendelea) kwamba eti mazoezi ni
suala la ujana; kumbe kadri unavyokuwa ki umri ndivyo kadri unavyotakiwa
kufanya mazoezi na kujitazama zaidi kiafya.
Watazame Wachina na Wajapani wanavyoishi maisha marefu.
Mazoezi ni shughuli inayokufanya kwanza uheme (mapafu na moyo kwenda
kasi), viungo na mifupa kujinyoosha (stretching), kutoka jasho na
usafishaji wa damu. Mazoezi yanayosaidia haya ni pamoja na kutembea
kasi, kukimbia, kuogelea, michezo mbalimbali ya riadha (kama mpira wa
miguu, nyavu, kikapu, mikono, nk); michezo ya kupigana na kujilinda
yaani masho ati(karate, kung fu, judo, capoeira, krav maga, jiu jitsu,
systema, kickboxing, thai boxing, kempo, kalari payatu, aikido, nk) …
Ni muhimu mwanadamu ufanye mazoezi makali ya viungo mara mbili tatu
kwa juma. Si vizuri kufanya kila siku kwani musuli na mishipa inahitaji
kupumzika na kukua.
Kama unapenda kuinua vyuma lazima uwe na mwalimu wa kukuelekeza; na
si vizuri kufanya kila siku. Wastani wa mara mbili tatu kwa juma
inatosha kabisa.
Mdau
wa Kitoto naikabili bahari shakiri ya English Channel. Kuogelea ni moja
ya tizi bab kubwa lisilohitaji kingine bali mwili wako...maji bure
asilia ya Muumba al Dunia. (Picha na A. Macha)
6-UPO UFANYAJI MAZOEZI WA AINA MBILI
Mazoezi ya nguvu ya kuhema niliyotaja hapo juu (cardio-vascular) na
yale laini ya kujinyoosha yaani ambayo hutumia zaidi nguvu za ndani na
pumzi. Haya ya pili ni kama Yoga (India) , Tai Chi Chuan (China) na aina
mpya mazoezi iliyoanza Majuu miaka ya karibuni yaani Pilates (hutamkwa
hivyo hivyo ilivyoandikwa Pilates). Haya laini yanawafaa zaidi watu
wazima na nchini China na Japan mathalan utawakuta wazee wa miaka 80
hadi 90 bado wanayafanya. Husaidia moyo, damu na akili.
Michezo na mazoezi ya mwili ni njia kuu ya kupunguza unene, kurefusha
maisha, kuchangamsha ubongo, kupunguza ulevi, uvutaji sigara, dawa za
kulevya, tabia mbaya za uvivu, ugomvi, nk. Mataifa yenye watu
wanaofanya mazoezi kama Japan, Brazili, India, China nk huwa na wachapa
kazi wengi na wananchi wanaoipenda jamii yao.
Chakula
cha wanga kwa wingi kilichozoeleka sana Afrika ni kitamu; ila kinakosa
mboga mbichi za majani, yaani Saladi- (Picha na F Macha)
7-KULA SANA CHUMVI SI VIZURI
Ulaji chumvi mwingi hutokana na suala la ladha. Kisayansi vyakula
vyote vina chumvi asilia sema tu tumezoea kuongezea madini hii iitwayo
Sodium. Sodium inachangia sana kufupisha maisha. Huifanya mishipa ya
damu ichoke; ni kama bomba lolote la maji ukilitazama baadaye hugeuka
rangi kutokana na yale maji kupita pale kila siku.
Kwa wale tunaoishi nchi za joto na kutoka sana jasho kula chumvi ni
muhimu. Ila tatizo letu ni kwamba hatunywi maji ya kutosha. Mtu ukiwa na
kiu unakunywa soda au kinywaji cha sukari; inakuwa kama unaendelea
kuutesa mwili. Kwa vipi? Mishipa inayopitisha damu mwilini badala ya
kusaidiwa kwa maji inawekewa kazi zaidi ya kusafisha sukari na chumvi.
Ndiyo maana vifo vingi vinatokea mapema; wastani wetu wa maisha haupiti
miaka 50.
Utafiti uliofanywa chuo kikuu cha California, Marekani mwanzoni mwa
2010, umethitibisha kwamba vifo vingi duniani husababishwa na maradhi ya
moyo na saratani ambavyo hutokana na uvutaji sigara, unene, ulevi na
ulaji sana wa chumvi na sukari. Tukipunguza ulaji wa chumvi tunasaidia
pia kupunguza maradhi ya moyo, utafiti unasema.
Mabasi
ya ghorofa daraja mashuhuri la Tower Hill, London. Asilia kubwa ya
wakazi hapa wanahusudu sana mazoezi shauri mji umebanana sana na hewa si
safi. Taswira ilipigwa na mpiga picha Mike Nicholas, baharia wa Kibongo
mkazi, Denmark, alipotembelea jiji hili la nne duniani kwa gharama,
karibuni .
8-TAFITI ZA VYUO KADHAA ULIMWNGUNI KUHUSIANA NA AFYA
-Jarida la Kimarekani la sayansi lilieleza mwaka jana kwamba
utapunguza ugonjwa wa moyo (ambao husababishwa na unene , wasiwasi na
purukshani) kwa asilia mia 42 kama utakula matunda na mboga za majani
peke yake kila siku, juu ya msosi wa kawaida.
(PENDEKEZO LA KULA- Na 4- Kula mlo wako. Baada ya saa mbili au
tatu, sakatia tunda au matunda; baada ya mlo mwingine, kula sahani ya
mseto wa mboga mbichi kama karote na matango. Utaona tofauti ya afya,
ngozi, wajihi, kinyesi, usingizi, nk. Kidesturi tumezoea kunywa chai au
soda za sukari sukari na gesi kati kati nya milo badala ya matunda na
mboga mbichi za majani).
-Utafiti uliofanywa na wanasayansi chuo kikuu cha South Carolina mwanzo wa mwaka 2010 kuhusu faida za kuogelea.
Zoezi la kuogelea lina faida zaidi ya kukimbia au kutembea kwa vile
huchanganya mazoezi makali na pumzi, kusaidia mapafu na moyo. Utafiti
ulithibitisha kuogelea hupunguza hatari za kifo kwa asili mia hamsini.
-Utafiti wa jarida la chuo cha uganga Ulaya umeeleza (desemba 2009)
kwamba kulala nusu saa kila mchana (“nap”) husaidia kupunguza ugonjwa
wa moyo kwa asilimia 37.
-Uchunguzi wa chuo cha michezo cha Hispania mwanzoni mwa 2010
umethibitisha kwamba ukikimbia mara tatu kwa juma (jogging) unaongeza
nyege mwilini kwa asili mia 75. Hasa kwa watu wa makamo mnaoanza
kupoteza nguvu za urijali.
-Uchunguzi chuo kikuu cha Leeds, Uingereza mwanzoni mwa 2010
umeonyesha unapotembea kwa miguu, ukikwepa barabara kubwa zisisokuwa na
mioshi ya magari (pollution) unapunguza matatizo ya maradhi ya hewa
chafu kama pumu, mapafu na appendix.
-Uchunguzi wa chuo kikuu cha Texas mwaka 2010 umegundua kwamba kula
tunda la divai nyekundu mara kwa mara husaidia kupunguza kupata ugonjwa
wa kisukari.
-Hapo hapo tunaelezwa kwamba watu weusi na bara la Asia wanakumbwa
zaidi na ugonjwa wa kisukari kutokana na vinywaji vya sukari sukari na
gesi (fizzy drinks). Ukinywa kiasi cha miligramu 300 za vinywaji hivi
(Cocacola, Red Bull, Fanta, nk) kwa siku unajitahadharisha kupata
kisukari.
Njiwa
London, mtaa wa Westbourne Park. Huruhusiwi kisheria kumpiga manati,
kumuua au kumfanya ndege huyu kitoweio nchi hii. (Picha na F. Macha)
9-KUFUNGA
Neno kufunga linatambuliwa rasmi kuhusiana na Waislamu (mwezi
Ramadhani) au Wakristo (Lenti nk). Ufungaji huo una masharti mengine ya
kidini tofauti na haya ya kiafya.
Mathalani wafungaji hawa hula chakula kingi usiku; ukihesabu
wanafunga wastani wa saa 12 tu. Kawaida ukitaka virusi na takataka
nyingine mwilini zitoweke, au viungo vipumzike wahitaji saa 20
kuendelea.
Ufungaji ninaouongelea ni ufungaji wa kutokula kabisa kwa saa 24, 36 hadi 48 kuendelea…
Ufungaji ni nini?
Kama mashine yeyote mwili wa mwanadamu unahitaji kupumzika na
kujisafisha. Hata tukiwa tumelala bado viungo mbalimbali mwilini
vinafanya kazi. Kwa hiyo faida ya kwanza kabisa ya kufunga ni
kuupumzisha mwili kama mfanyakazi yeyote anapokwenda likizo.
Faida ya pili ya kufunga ni kusafisha mwili kutokana na uchafu ambao
haukutoka (kinyesi hakitoi mabaki yote toka utumbo mkubwa), dawa na
takataka za mazingira tunayoyavutia hewa, virusi au kuyanywa katika maji
na vyakula mbalimbali na pia uchafu wa hisia, yaani hasira, huzuni, nk.
Kuna ufungaji wa aina mbalimbali.
1-Kufunga kwa kunywa maji tu, saa 24 kuendelea…
2-Kufunga kwa kutokunywa maji au kula chochote, saa 24 kuendelea…
3-Kufunga kwa kula tu matunda au mboga zilizopondwa kama karote, matango nk, saa 24 kuendelea…
Ufungaji huu unatakiwa ufanywe kwa mpangilio. Kitu muhimu si tu
kufunga bali NAMNA unavyofungua. Ukianza kula tena, unaanza taratibu.
Kawaida ni vizuri kuanza na maji, kikombe au bilauri ya kwanza taratibu.
Subiri tena nusu saa, bilauri nyingine, halafu hadi ya tatu, halafu
ndiyo matunda yasiyo ya chachu, na kadhalika. Kuanza kufungua kwa kunywa
chai ya maziwa, uji au vyakula vingine vya wanga hakusadii sana mfungo
huu.
Maana lengo lake ni kusafisha mwili.
PENDEKEZO LA 5- Kwa wenye imani za kidini. Unaweza pia kufunga
hivi ukawa pia unasali au kuvaa mavazi yanayokufanya mtu wa amani.
Ukifanya hivi unajitakasa kimwili na kiroho. Si lazima ungojee ile miezi
ya kufunga na wengine.
10-USINGAJI
Usingaji au masaji ni njia nzuri sana ya kupunguza unene. Ikiwa
unaangalia namna unavyokula, unafanya mazoezi na kusingwa mara moja au
mbili kwa mwezi unaupalilia mwili vizuri. Nini faida ya usingaji?
Kusinga husaidia ngozi, mishipa ya damu na sura nzima ya mwili na
taswira yako mwanadamu. Wengi wetu tunaposikia neno kusinga tunafikiria
usingaji wa mapenzi. Hivi ni vitu viwili tofauti kwani usingaji wa
mapenzi unaimanisha mahusiano ya kihisia.
Kifupi mwanadamu unatakiwa uwe unautunza na kuungalia mwili wako kama
nyumba au hekalu lako. Wengi wetu tunaoga, tunajipaka marashi,
tunasuka, tunanyoa nywele au ndevu; lakini miili yetu kiundani inaoza
taratibu…
NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI YA KUONDOA TUMBO NA KUPUNGUZA MAPAJA
Jinsi ya kuanza mazoezi ya tumbo na namna ya kumalizia
- Jiulize ni kwanini unataka kufanya mazoezi?
- Panga muda wako mzuri ili usigongane na shuguli nyingine muhimu za kimaisha.(Asubuhi na mapema Recommended)
- Hakikisha mwili wako ni mzima kiafya(huna maleria na magojwa mengine yakawaida)
- Tengeneza ratiba yako ya mazoezi,(siku ngapi na ni mazoezi gani utafanya)
- Kuwa na malengo(baada ya mwezi mmoja nataka niwe nimepungua kilo 2 mfano)
- Hakikisha unapima kilo zako kabla ya kuanza mazoezi(hukutia moyo ukijua umepungua)
- Anza kidogo kidogo(yani inaweza kuwa mara 3 au 4 kwa wiki ila iwe ni zaidi ya 30 mnts)
- Pata muda wa kupumzika vyakutosha.
Ningependa
kushauri kwamba kwa wale wote ambao ndio mara ya kwanza wanaanza
mazoezi ya kupungua kwa mwezi wote wa kwanza wafanye mazoezi ya kukimbia
tuu na kunyoosha viungo(ingawa zoezi sio kukimbia tuu hata kuogelea ni
zoezi kubwa sana nafikiri ndio zoezi number moja duniani linalopunguza
uzito haraka zaidi kuliko mengine kwa mujibu wa wachunguzi) ili kuupa
mwili taharifa ya nini kinakuja au kuaandaa mwili kwa lugha nyingine
wakati huo pia unatengeneza na pumzi yakukusaidia katika mazoezi
yanayofuata baada ya hapo.
Chini kabisa ni mazoezi ya mapaja
kuanza na kumalizia
EVANSKISAYE
AINA YA MAZOEZI
Mara nyingi sana katika maisha watu wengi hupata tatizo la kuwa na tumbo
kubwa na baadae humletea madhara. Ili kuepuka tatizo hili ni kuamua
kufanya mazoezi kupunguza ya mafuta katika chakula na kufanya mazoezi
ya tumbo hii ndio njia pekee hakuna njia mbadala.
Zoezi hili ni kufanya kwa kutumia mashine(abs board)
Hapo ni zoezi ambalo utumia mpira maalum. uanzapo;
Zoezi la mpira maalum umaliziapo kwa kunyaua juu.
Hapa ni mazoezi ya tumbo kwa kutumia mpira maalum
Kwa kutumia bench la zoezi la tumbo unavyoanza
Namna unvyomalizia zoezi kwa kunyanyuka.
Zoezi la tumbo kwa kutumia hypic chair unavyoanza.
Zoezi la tumbo unavyomalizia kwa kutumia hypic chair
Zoezi la aina nyingine kwa kutumia mpira wa zoezi hilo
OMARYSWAI
au ukiona hayo yote unashindwa nunua
berring kisha nenda kwafundi akuchomelee chuma baada yahapo utakuwa
unafanya mazoezi chumbani kwako kwakutumia hiyo berring..