PATA HABARI KAMILI YA MAZISHI WA WALIOKUFA KUTOKANA NA MLIPUKO WA BOMU OLASITI ARUSHA
0
Leo ilikuwa nisiku nyingine ya majonzi
ambapo maelfu ya watu walijitokeza wakiwa na nyuso za huzuni na majonzi
tele kuwapumzisha ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki kutokana na
mlipuko wa bomu uliotokea jpili iliyopita ambapo mpaka sasa watu watatu
wameshafariki na ndo hao leo wamezikwa kwa heshima kubwa mbele ya kanisa
la katoliki huko olasiti..
Waliokumbwa na mauti kutokana na mlipuko wa bomu hilo ni Mama Reginald loning'o laizer aliyezaliwa mwaka 1963 mkazi wa olasiti ambaye ameacha mume na watoto saba.
JAMESGABRIEL KESSY aliyezaliwa Majengo
Arusha mwaka 1997 aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya
sekondari ya Arusha Day. amewacha wazazi wke na watoto wenzake watatu.
PATRICIA JOACHIM ASSEY aliyezaliwa
Majengo Arusha mwaka 2003.ameacha wazazi wake ambapo mama yake mzazi
amelazwa Hospitali ya Muhimbili akipata matibabu zaidi baada ya
kujeruhiwa na bomu siku hiyo..
KIPEPERUSHI CHENYE PICHA ZA MAREHEMU WOTE NA WASIFU WAO..
Ifuatayo ni habari fupi pamoja na picha ya yale yote yaliyotokea katika mazishi hayo.
1-Watu walifika kanisani tayari kabisa kwaajili ya kupokea miili ya marehemuu
2-Kuingia kwa wageni rasmi
WAGENI RASMI WALIOHUDHURIA NI
1.Waziri mkuu Mizengo Pinda
2.waziri mkuu mstaafu mh. Edward lowassa
3.Waziri nchimbi
4.Mwenyekiti wa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe
5.Mwenyekiti Wa NCCR-MAGEUZI ndugu JAMES MBATIA
5.Mkuu wa mkoa wa arusha ndugu mulongo
6.Mbunge wa Arusha mh. Godbless Lema
7.Viongozi kutoka serikali ya Zanzibar
8.Wabunge mbalimbali
9.viongozi wa dini mbali mbali akiwami shekhe mkuu wa Arusha,Viongozi wa dini ya kihindu
10.pamoja na viongozi mbalimbali wa usalama wa Taifa
3-Miili ya marehemu kufika kanisani na
kuingizwa kanisani ambapo kwaheshima kubwa kabisa miili yote iliingizwa
na viongozi wa katoliki.
4-Baada ya miili kuingizwa Kanisani Misa ya Kubariki kanisa jipya ilianza ikiwanipamoja na kunyunyuzia maji ya baraka.
4-Ilifanyika ibadamaalum ya kuwapokea Marehemu wote watatu ndani ya kanisa.
5-kwaya nayo ilipewa nafasi ya kuimba
6-kisha ibada baada ya ibada Baba Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu alikaribiswa kutoa neno ambapo alianza kwa kuwashukuru watu wote
7- Baada ya neno kutoka kwa askofu mkuu wa Jimbo la arusha watu waliungana kutoa Sadaka.
8-Kilichofuatia ilikuwa nikusomwa kwa wasifu wa marehemu wote Mama Regina,Patricia na James.
9-Kisha Ulifika wakati wa salamu za rambirambi kutoka kwa viongozi mbalimbali wa dini na waserikali.
Wakwanza kutoa salamu za rambirambi alikuwa ni ndugu Ngalale Kumtwa ambaye ni kiongozi wa baraza la Maaskofu. kama
ilivyo alianza kwakutoa pole kwa wafiwa wote kisha alinza kulalamikia
vitendo viovu hasa vya kidini dhidi ya Wakristo hapa Tanzania,
aliendelea kuelezea kuwa kwasasa mahusiano baina ya Waislamu na Wakristo
unazidi kuzorota pia aligusia na kuelezea kuhusu mkutano mkubwa wa
baadhi ya waislamu ambao ulifanyika Daresalam katika ukumbi wa Diamond
Jubilee uliofanyika mwaka 2011 ambapo waislamu walidai
kuwa serikali inawapendelea sana wakristo, alizidi kuelezea kuwa baadhi
ya waislamu hao waliafikia kufa ama kuua kwaajili ya kueneza uislamu na
kuungamiza ukristo hapa Tanzania. Pia aliilamu sana serikali kushindwa
kukemea nakudhibiti matukio hayo.. Aliomba vyombo vya dola kuchimba
ndani zaidi na kuwafahamu wahusika wote wanaoeneza vita hivi vya udini
na kuwakamata kisha kuwafikisha mbele ya sheria..
Wapili alikuwa ni Baba Askofu drAlex Malasusa
kama ilivokawaida naye alianza kwakutoa pole kisha aliwawafariji wafiwa
wote na kuwapa moyo kwa kuwaambia ya kuwa risasi,mabomu na uchomaji wa
makanisa visitukatishe tamaa wakristo kwani ukristo upo katika mioyo
yetu alizidi kusema kuwa siku ya mwisho hatutihukumiwa kwa mabaya tuu
bali tutahukumiwa kwa yale mema ambayo hatukuyatenda hapa duniani.
Salamu za tatu za rambirambi zilitoka kwa UMOJA YA MADHEHEBU ARUSHA ambapo mjumbe alitoa pole na pia alisema kuwa jambazi hana ndugu na nchi hii niya watu wote na hakuna dini yenye chama.
Salamu za nnezilikuwa zitoke kwa shekhe mkuu wa BAKWATA ila
aliondoka baada ya ibada kwani alienda sehemu nyingine kwaajili yamaziko
mengine.
Salamu Ya tano na mwisho kabisa ilitoka kwa MH. Mizego Pinda ambaye niwaziri mkuu wa Tanzania aliyetoa salamu kwaniaba ya serikali na viongozi wote.. Kama
ilivyoalianza kwakutoa salamu zake za pole kwa wafiwa wote na
Watanzania wote kwaujumla..Neno kubwa la waziri mkuu nikuwa hakuna
aliyetarajia mauti ila ndo hivyo mauti yamewakumba marehemu hao kwahiyo
nilazima tukubaliane na hilo na tuwaombee ili walazwe mahali pema peponi
pia waziri mkuu hakuishia hapo alisemma ya kuwa kuua mkristo mmoja au
kiongozi mmoja sio kukomesha ukristo, ukristo na uislamu unahistoria
kubwa sana na utakuwa unajidanganya kuwa ukiua mufti mmoja utakuwa umeua
uislam. Dini hizi zote mbili zina nguzo ndefu sana.. Katika kumalizia
waziri mkuu alitoa msimamo waserikali kwa kusema kuwa serikali
itapambana na kukomesha kundi hilo linalosababisha vita vya kidini
nchini.Pia ameamrisha ofisi ya mambo ya ndani kufanya kazi ya ziada
kukomesha uhalifu huu na aliwaomba wananchi wote wasaidiane na polisi
kutoa taarifa juu ya wahalifu wote na serikali itawakamata na
kuwafikisha mbele ya sheria.. Katila kumalizia waziri mkuu alimalizia
kwa kutaja kiasi cha rambirambi alichokabidhiwa ambapo nijumla ya
milioni 12,kumi zikitoka benki ya NMB namillioni mbili zilitoka
kwabbadhi ya viongozi ambao alifanya nao kikao cha serikali ya vitongoji
ambao wao binafsi walijichanga hapohapo na kupatikana kwahizo milioni
mbili..pia ofisi ya waziri mkuu ilitoa sh.millioni mia 100,000,000 pia
serikali itagharamikia matibabu yote na hata ikitokea majeruhi akahitaji
matibabu nje ya nchi serikali itagharamikia mataibabu hayo..
10-Baada ya salamu za rambirambi ilifuatia nenpo la shukrani ambalo
lilitolewa na Askofu Mkuu Lebulu.alianza kwa kutoa pole kisha alitoa
shukrani kwa watu wote wakiwamo viongozi wote wadini na
serikali,viongozi ya serikali ya Zanzibar waliofunga safari hadi katika
eneo latukio,hospitalini nasiku ya mazishi pia,viongozi wa BAKWATA
uliowawakilisha waislamu wote Tanzania,viongozi wa dini ya Wahindu na
viongozi wote wadini wanao thamini na kujali utu wa binadamu pia alitoa
shukrani kwa wanaOlasiti wote,WanaArusha,Waaumini wote na Watanzania kwa
ujumala walishiriki kwa hali na mali katika tukio hili tokea siku ya
mlipuko hadi leo hii..
11-Mwisho kabisa ilikuwa ni shughuli nzima ya kwenda kuwapumzisha salama
ndugu zetu wote waliotutoka kutokana na mlipuko wa bomu..
ZIFUATAZO NI BAADHI YA PICHA ZIKIONESHA TUKIO ZIMA ILIVYOKUWA..
MAGARI ZILIZOBEBA MIILI YA MAREHEMU IKIWASILIA NJE YA KANISA
WAZIRI MKUU MSTAAFU MH.EDWARD LOWASSA AKIWASILI KANISANI
MH. JAMES MBATIA AKIWASILIA KANISANI
MAPADRI WAKIJIANDA TAYARI KABISA KWAAJILI YA KUBEBA MAJENEZA YENYE MIILI YA MAREHEMU WOTE
PICHA ZIKIONESHA UMATI WAWATU WALIOFIKA KUJA KUZIKA
MUONEKANO WA KANISA KWA NDANI
ENEO BOMU LILIPOTUA
WAZIRI NCHIMBI AKIWASILIA
MAJENEZA YALIYOBEBA MAREHEMU WOTE YAKIWA NDANI YA KANISA