Mtoto mwenye miaka 8 afariki kutokana na majeraha ya ngono usiku wa harusi yake akiwa na mume wake alie na mara tano ya umri wake

0


Bibi harusi mtoto mwenye umri wa mika 8 amefariki dunia usiku wa harusi yake baada ya mateso ya majeraha ya ndani kutokana na kiwewe ngono (Sexual trauma). 
Kifo kilitokea katika eneo la kikabila la Hardh kaskazini magharibi mwa Yemen, ikipakana na Saudi Arabia.


Haki za binadamu imeshatoa wito kwa kukamatwa kwa mume wake ambaye alikuwa mara tano ya umri wa mtoto huyo.habari hii imeleta attention zaidi kutokana na kuwepo kwa ndoa za kulazimishwa kwa watoto katika kanda ya mashariki ya kati.
"Kutokana na Umoja wa Mataifa ya Idadi ya Watu (UNFPA), kati ya 2011 na 2020, zaidi ya wasichana  milioni 140 watakuwa wanaharusi watoto,  Aidha katika wasichana hao milioni 140 ambao wataolewa kabla ya umri wa miaka 18, milioni 50 watakuwa chini ya umri ya 15. "

Na imeripotowa kwamba zaidi ya robo ya wasichana Yemen wanaolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 15, na hali hii, si tu hufanya wao kukosa afya na elimu, bibi harusi hao watoto wanakabiliwa na vurugu ya kimwili, kihisia na kijinsia katika ndoa zao za kulazimishwa.

Mwaka 2000 sheria Yemen iliunda sheria iliyopitisha umri wa miaka 17 kuwa ndio umri wa msichana kuolewa, lakini bahati mbaya idadi kubwa ya wabunge wa kihafidhina kudai kuwa ni kinyume na uislam.

HUU NI UNYAMA UNYAMA UNYAMA ULIOPITA MAELEZO!!  MTU ANAWEZAJE KUOA MTOTO WA MIAKA NANE??  DUNIA IMEKWISHA, NA HAO WAZAZI WA HAO WATOTO WANAKUWA WAMELALA USINGIZI WA AINA GANI??
SHAME SHAME SHAAAME!! 

0 comments: