Ommy Dimpoz Akiwa Houston Texas

0
Jana Ommy Dimpoz alikuja Houston Texas ikiwa ni mmoja wa miji kadhaa atakayo itembelea akiwa katika ziara yake ya Marekani, alituburudisha sana, ingawa alichelewa sana kuingia ukumbini lakini alipoingia aliwasuuza mioyo washabiki wake na mimi nikiwa mmoja wapo. Ilikuwa patashika Nguo kuchanika.. Mauno yalikatwa hapo balaaa hahahaha.. 

Tatizo ni moja tu wasanii wetu kutoka Tanzania wakiwa wanakuja huku nchi za nje huwa hawaleti CD zao. 

Nilifanikiwa kumuuliza Ommy Dimpoz kama ameleta CD zake ili ni nunue kwa sababu mimi ni mshabiki wake mkubwa ningependa kuwa na CD ya nyimbo zake, Ommy Dimpoz kwa pozz alinijibu kuwa alipokuwa airport hakukubaliwa kusafiri nazo. Hilo ndilo lilikuwa jibu lake Mr. pozz kwa pozz.

We had so much fun... 


Ommy Dimpoz did his thing jana.. Yaani alituburudisha sana..

0 comments: