DIAMOND: NILISHAWAHI MKUTA WEMA AKIWA UCHI NA MTU MWINGINE HOTELINI.

1

WALIPENDANAGA HAWA JAMANIII!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Baada ya kuamua kutokaa kimya kutokana na shutuma zilizotolewa dhidi yake na mpenzi wake wa zamani WEMA SEPETU, Mwimbaji DIAMOND PLATNUMS ameamua kutoa kauli yake ya mwisho kuhusu Wema.
Diamond anakiri kwamba hakutaka kabisa kumzungumzia Wema kwenye vyombo vya habari baada ya kuachana kwa sababu hakutaka malumbano lakini imebidi iwe hivyo kwa sababu ya hasira aliyoipata kutokana na Wema kuzungumza uongo mwingi dhidi yake.
Exclusive na millardayo.com Diamond amekiri kwamba aliachana rasmi na Wema mwezi january mwaka huu na hiyo ni kutokana na kukerwa na tabia za Wema alizozikemea lakini mwisho wa siku hakufanikiwa, zikawa zinaendelea…. ambapo tabia hizo ni pamoja na Wema kuwalipa waandishi wa habari wa magazeti ili watoe stori zake, japo Diamond alikua anawalipa waandishi wasiandike chochote, yeye alikua anawalipa zaidi.
Diamond amesema “kuna vitu vya chinichini alikua ananifanyia vya kuniumiza kama kudanganyana lakini nilikua sivipeleki kwenye vyombo vya habari kwa sababu nilikua namuheshimu namfichia kwa sababu anasema hafanyi hivyo, lakini akawa anaendelea kuvifanya kama kunidanganya kwenye mapenzi japo kudanganyana kwenye mapenzi ni kitu cha kawaida hata wapenzi wangu wa zamani walikua wananidanganya na mimi nawadanganya pia, lakini alikua anapeleka kila kitu kwenye magazeti hata vitu vya watu wawili ndani ya nyumba anavipeleka, sasa nyumba inakua haina siri”
Ameamplfy zaidi kwamba “Wema alikua anapeleka stori kabisa yani kitu tumefanya watu wawili ndani unashangaa kukikuta kwenye gazeti, nikikutana na waandishi ambao ni rafiki zangu wananiambia ebwana wewe unajisumbua bure yeye mwenzako akija hapa ndio anataka aandikwe, mimi nilishawahi kumkuta hotelini uchi kabisa akiwa na mwanaume mwingine hotelini mwishoni mwa mwaka jana lakini sikuongea chochote kwenye vyombo vya habari, nikamchukua na kuondoka, niliamua kumtunzia siri yake na nikanyamaza kwa kuichukulia kama mwanaume, na hata nikawa nikifika kwenye media nilikua nampamba na kumtetea kwamba jamani Wema hayuko hivyo na ni mstaarabu”
Diamond amefunga mjadala wa yeye na Wema kwa kuthibitisha kwamba hana ugomvi na Wema wala hana tena hisia za kimapenzi kwa mshindi huyo wa Miss Tanzania 2006, hawezi kurudiana nae kwa sababu kwa sasa imetosha na anampenzi mwingine ambae hata Wema anamfahamu.
Ishu yote hii imetokana na show aliyoifanya Diamond pale Mlimani City weekend iliyopita ambapo Diamond alikataa kupokea pesa Wema Sepetu aliyokua anampa pale kwenye stage kwa sababu ya kukwepa Drama, Na Wema hakua mpenzi pekee wa zamani wa Diamond aliekuwepo kwenye show, kulikua na warembo wengine wawili wa zamani wa Diamond lakini hao wote alipokea pesa zao.
Uhusiano wa Diamond na Wema umedumu kwa mwaka mmoja ambapo walipanga kuoana huku tayari Diamond akiwa amemvisha pete ya uchumba mrembo huyo ambae pia ni mwigizaji wa movie Tanzania.
Diamond amethibitisha kwamba Show yake ya DIAMONDS ARE FOREVER siku tatu kabla ya kufanyika, tayari ilikua imeuza ticket zote elfu moja na hivyo ukumbi kujaa, huku kila ticket ikiwa ni shilingi elfu 50…… show yake imekua show ya kwanza ya msanii wa kibongo kulipisha watu elfu 50 na bado ikajaza mapak watu wakakosa ticket, kwa swala la kiingilio amezishinda mpaka show za Jay Z & 50 cent ambazo zilifanyika bongo na watu kulipa elfu 25 – 30.

1 comment:


  1. am Dr Amigo. I can cast a spell on your behalf regarding a relationship, your financial situation, future events, or whatever is important to you. I have the power and I use the power. I can change the course of your destiny. Contact me and I shall cast a spell for you. Tell me what it is you want and I shall go about my work. Is it someone or something you desire to have? Do you want wealth, or happiness, or a mate E.T.C.
    Lost lover specialist
    1. We bring back lost lover
    2. Do you want to win your loved one
    3. We help single people to find partners
    4. Do you want to be married?
    5. Love attraction.
    6. Married problems & Divorce
    8. Love portion
    9. Have a straight friend that you want? The i can help you out

    All these done in 1 - 7 Days, Privacy place strictly
    confidential Result 100% Guaranteed and i have divine powers that enable you to connect to your forefathers or ancestors to give you guidance in life and enable you to change the course of your destiny
    To inquire about my services, contact me by phone, e-mail. I will be happy to assist you 24 hours a day, 7 days a week. For an immediate response please contact me by
    Call/Whatsapp +2349058764985
    Email: dr.amigo71@gmail.com
    Dr Amigo.

    ReplyDelete