CHRIS BROWN KAM-DUMP GIRLFRIEND WAKE.

0
.
 Chris Brown ametangaza rasmi kuachana na mpenzi wake ambae ni Karrueche, kwenye tamko alilolitoa amenukuliwa akisema “nimeamua kuwa peke yangu ili kuzingatia career yangu, nampenda Karrueche sana lakini sitaki kumuona akiumia kutokana na urafiki wangu na Rihanna, ni bora niwe single ili sisi sote tuwe na amani kwenye maisha yetu”
Kwa miezi kadhaa sasa hivi Rihanna na Chris Brown waliokua wapenzi zamani wameripotiwa kurudiana kwa siri ambapo mara nyingi taarifa zao na picha zimekua zikivuja ishu ambayo inawafanya wengi waamini wamerudiana, na ni tabia ambayo inadaiwa imekua ikimuumiza sana Karrueche kwa sababu bado anampenda na anahitaji kuendelea kuwa na Chris Brown.

0 comments: